Baada ya kupata hasara kwa takribani miaka 10, hatimaye klabu ya Chelsea inatarajia kutangaza faida ya £20m kwa mwaka wa fedha wa 2013/14. Faida hii imechangiwa na mauzo ya wachezaji David Luiz na Juan Mata.
Mapato ya mwaka mzima kwa Chelsea yalikuwa ni £325m na kutokana na faida waliyoingiza sasa watakuwa wamekivuka kikwazo cha sheria ya kanuni ya matumizi ya fedha kwa vilabu – UEFA’s Financial Fair Play (FFP).
Chelsea walimuuza Juan Mata kwa £37 kwenda Man United wakati dirisha la usajili la January mwaka huu, kabla ya kumuuza kwa faida kubwa David Luiz kwa ada ya uhamisho wa £50m na huku wakipata mgawo mzuri kutoka kwenye dili jipya la haki ya matangazo ya TV lenye thamani ya £1billion.
Rekodi zinaonyesha tangu timu hii iliponunuliwa na tajiri wa kirusi Roman Abramovich miaka 10 iliyopita wamekuwa wakipata hasara – jambo ambalo liliwaweka hatarini kuwa miongoni mwa timu zilizokuwa zikidhibitiwa na FFP.

2004 – Loss £74.7m
2005 – Loss £131.6m
2006 – Loss £77.1m
2007 – Loss £65.6m
2008 – Loss £69.2m
2009 – Loss £45.8m
2010 – Loss £69.2m
2011 – Loss £70.7m
2012 – Profit £1.4m
2013 – Loss £49.4m








0 comments:
Post a Comment