Friday, November 14, 2014

RONALDO AKABIDHIWA TUZO YA DI STEFANO KWA MARA YA TATU MFULULIZO

ronaldoMshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo jumatatu hii alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa ligi kuu ya Hispania tuzo hiyo ya Heshima inajulikana kama tuzo ya f Alfredo Di Stefano.
Ronaldo alipokea tuzo hiyo huku akisikitikia kutokuwepo kwa gwiji Alfredo Di Stefano ambaye aliefariki dunia mwezi July kwa ugonjwa wa mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 88.
Nyota huyo wakimataifa wa Argentina aliisaidia Madrid kutwaa mataji matano makubwa barani ulaya kuanzia mwaka 1956-60. Alitwaa tuzo ya mwanasoka bora barani Ulaya mwaka 1957 na 1959, mwaka 2000 alitajwa kuwa ndiye rais wa heshima wa klabu ya Madrid.
Rais wa Madrid Florentino Perez siku ya jumamosi juma lililopita alimfananisha Ronaldo na Di Stefano.
Ronaldo alifunga magoli 31 kwenye La Liga , ambapo Madrid walimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid pamoja na Barcelona.
RONALDOOO
Ronaldo ameanza vizuri msimu huu kwa kufanikiwa kufunga mabao 23 kwenye michezo 17 alioichezea Madrid, anapewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya FIFA Ballon d’Or . kwenye la liga anaongoza kwa kuwa amefunga mabao 18 mpaka sasa.
washindi watano wa tuzo ya DI STEFANO katika miaka mitano ni
2009-10 Lionel Messi
2010-11 Lionel Messi
2011-12 Cristiano Ronaldo
2012-13 Cristiano Ronaldo
2013-14 Cristiano Ronaldo

0 comments:

Post a Comment